IQNA

Waumini  500 washiriki kikao cha Khatm Qur’ani nchini Algeria

23:45 - December 31, 2024
Habari ID: 3479982
IQNA – Wanaume na wanawake mia tano waliohifadhi Qur’ani Tukufu kutoka mikoa mbalimbali ya Algeria wamekusanyika kufanya Khatm Qur’ani katika kikao kimoja kama sehemu ya mpango wa kitaifa wa Qur’ani. Khatm Qur’ani ni usomaji wa Qur’ani kutoka mwanzo hadi mwisho.

Mpango huu ulifanyika Jumamosi, Desemba 28, 2024, kuanzia baada ya Swala ya Alfajiri hadi Swala ya Magharibi, ambapo washiriki 500  waliweza kusoma Qur’ani Tukufu kikamilifu. Katika chapisho la Facebook, Taasisi ya Harakati za Qur’ani ya Algeria ilisema kuwa baada ya karibu miezi tisa ya maandalizi na ushirikishwaji wa wanafunzi elfu moja katika hatua za awali za mradi, washiriki 500 wenye ustadi walifikia siku hii ya kukumbukwa, wakionyesha mapenzi yao kwa Qur’ani na dhamira yao ya kuitumikia.

Programu kama hizi za Khatm Qur’ani zitaendelea kufanyika kila Jumamosi kuanzia Swala ya Alfajiri hadi Swala ya Magharibi katika vituo mbalimbali vya Qur’ani kote katika mikoa ya Algeria. Zitapeperushwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa Facebook wa taasisi hiyo. Wakati huo huo, raundi ya kwanza ya shindano la kusoma Qur’ani lililoitwa “Hafidh al-Wahy” (mwenye kuhifadhi ufunuo au Wahy) ilifanyika katika Msikiti wa Amir Abd al-Qadir katika mji wa Oran, Algeria Jumamosi, kwa ushiriki wa washiriki 100 wenye umri kati ya miaka 10 na 65. Raundi ya pili inatarajiwa kufanyika Aprili 2025, kulingana na waandaaji.

4256859

Habari zinazohusiana
Kishikizo: algeria qurani tukufu
captcha